Maisha ya Yesu

Pamoja na msimamizi • 16 masomo • 0 wanafunzi

Karibu kwa kozi ya ‘Maisha ya Yesu’! Tazama maisha ya Yesu kutoka Injili ya Luka, katika filamu iliyo tazamwa kwa wingi katika historia ya dunia. Kuna masomo 15, kila moja iko na kipande cha filamu hio, ikifuatiwa na maswali. Utapata mshauri wako binafsi ambaye atatoa maoni kuhusu majibu yako na pia unaweza kumuuliza maswali ya kufuatilia. Mshauri wako kawaida atajibu maswali yako ndani ya masaa 24-48.

Tunakushauri ufanye kati ya somo 1 au 2 kwa siku. Hii itakuwezesha kufikiria kwa kina yaliyomo kiroho kwa somo hili na kukuza uhusiano na mshauri wako kusemezana maswali yako na maisha yako ya kiroho. Itakusaidia zaidi kutumia wiki kadhaa kumaliza kozi nzima. Tunatarajia uandike majibu yote mwenyewe, bila usaidizi wa zana za AI kama ChatGPT.

Ni matumaini yetu utafurahia kozi hii na itakusaidia kusongea karibu na Mungu!

Anza kozi